Anthony Scaramucci,mmoja wa kikosi
cha mageuzi cha bw Trump,aliambia kipindi cha televisheni cha BBC HARDtalk
kwamba Sir Elton atawatumbuiza mashabiki mjini Washington DC mwezi Januari.
''Elton ataandaa tamasha wakati wa
sherehe za kuapishwa kwa bwTrump'', Scaramucci amesema
Lakini jambo hilo lilipingwa na
mwakilishi wa Sir Elton mjini London.
''Hakuna ukweli wowote kuhusu swala
hilo,'' aliambia BBC News.
Wakati wa kampeni ,Sir Elton alikuwa
akionyesha dalili za kumuunga mkono mpizani wa bw Trump,bi Hillary Clinton wa
chama cha Republican.
Akiwatumbuiza mashabiki katika
hafla ya uchangishaji wa pesa, ya bi Clinton mjini Los Angeles mwezi Oktoba,
aliripotiwa kuuambia umati kwamba: ''Tunahitaji mtu mwenye ubinadamu katika
ikulu ya White House,na siyo mtu mjinga''
Bw Trump alikuwa ametumia wimbo wa
Sir Elton Rocket Man and Tiny Dance bila idhini ya mwanamuziki huyo katika
kampeni zake.
No comments:
Post a Comment