Siku kadhaa baada ya utabiri wa TB
Joshua kuwa Hillary Clinton angeshinda urais wa Marekani kuwa tofauti, hatimaye
mhubiri huyo maarufu wa Nigeria ametoa ufafanuzi kuhusu kilichotokea.
Awali, TB Joshua aliwaambia waumini
wake kuwa aliona ndotoni kuwa Rais wa Marekani atakayechaguliwa atakuwa mwanamke
na kwamba atakumbwa na changamoto nyingi ikiwemo jaribio la kutaka kumuondoa
madarakani kwa kura za kutokuwa na imani naye.
Mhubiri huyo ametumia ukurasa wake
wa Facebook na Twitter kuutetea utabiri wake akidai kuwa Clinton alishinda
kupitia kura za jumla, kwa kupata kura nyingi zaidi ya Donald Trump.
“Tumeona matokeo ya uchaguzi wa
Marekani. Kwa kusoma, utagundua kuwa [utabiri]ule ulikuwa kuhusu kura za jumla
(popular votes), kura za wamarekani wengi,” unasomeka ujumbe
wa TB Joshua.
“Katika hali hii, tunahitaji roho
ya kinabii kutambua au kujua unabii. Viwango vyetu ni tofauti. Hatuko kwenye
viwango sawa. Tunaweza kuwa na makanisa makubwa, kengele kubwa, na shughuli
zote ambazo ni nzuri kwa viwango vya kibidamu lakini uwezo wa binadamu una
kikomo,” aliongeza.
Alitumia pia Biblia Takatifu kuupa
nguvu utetezi wake, akitaja maandiko ya 1 Wakorinto 1: 25, “Maana
kinachoonekana kuwa ni upumbavu wa Mungu, kina busara zaidi kuliko hekima ya
binadamu; na kinachoonekana kuwa ni udhaifu wa Mungu, kina nguvu zaidi kuliko
nguvu za binadamu.”
Clinton alishinda kwa kupata kura
nyingi zaidi za Wamarekani (popular votes) lakini alishindwa katika kura za
majimbo muhimu (electoral votes). Mgombea wa Republican ambaye tafiti nyingi
hazikumpa nafasi, alishinda uchaguzi huo na kuishangaza dunia.
Trump anatarajiwa kuapishwa rasmi
kuwa Rais wa Marekani, Januari mwakani.
No comments:
Post a Comment