Kwenye mahojiano ya kina na gazeti la New York Times la
Marekani, rais huyo mteule amenukuliwa akisema: "Nawashutumu sana.
Najitenga nao, na nawashutumu."
Alisema hataji "kuongeza nguvu" kundi hilo, ambalo
linajumuisha wafuasi wa sera za Nazi, watu wanaotetea ubabe wa Wazungu pamoja
na wanaopinga Wayahudi.
Nazi kilikuwa chama cha kisoshalisti kilichoongoza Ujerumani
wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia, na kililaumiwa kwa kutekeleza mauaji
dhidi ya Wayahudi.
Wafuasi wa makundi hayo walipigwa picha ya video Jumamosi mjini
Washington DC wakishangilia, mtu mmoja kwenye kipaza sauti aliposema:
"Hail Trump."
Nazi walimfurahia kiongozi wao Adolf Hitler kwa kuitikia
"Heil Hitler' na "Heil, mein Fuhrer".
Kwenye video hiyo, Richard Spencer, kiongozi wa kundi moja la
mrengo wa kulia, aliambia waliohudhuria kwamba Marekani ni ya watu weupe
(Wazungu) pekee, ambao aliwaita "watoto wa jua".
Aliwashutumu wanaopinga kundi hilo akisema ndio "viumbe
wabaya zaidi waliowahi kutembea katika sayari hii".
"Hail Trump, hail watu wetu, hail ushindi!" Spencer
anasema wakati mmoja, huku baadhi ya waliohudhuria wakiinua mikono yao juu na
kupiga saluti ya Nazi.
Mkutano huo wa Jumamosi uliwavutia waandamanaji walioziba
barabara kuzunguka jumba la Ronald Reagan, jumba la mikutano linalomilikiwa na
serikali katika mji huo mkuu wa Marekani.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alieleza wasiwasi Jumanne
kwamba ushindi wa Bw Trump uchaguzini huenda ukawapa matumaini watu wanaoamini
katika ubabe wa Wazungu.
Mmoja wa maafisa wake wakuu na wa karibu alisema video hiyo ya
"Hail Trump" inaogofya.
Lakini Bw Trump ameendelea kumtetea mwanamikakati wake mkuu
Steve Bannon, afisa mkuu mtendaji wa zamani wa Breitbart News, na akakosoa
madai kwamba tovuti hiyo ya kihafidhina ina uhusiano na kundi hilo
linalopigania ubabe wa Wazungu.
"Breitbart ni tovuti tu. Wanaandika habari kama vile tu
nyinyi pia huandika," ameambia New York Times.
"Kama ningefikiria kwamba yeye ni mbaguzi wa rangi au
kwamba anafuata mlengo wa kulia au baadhi ya hayo mambo, maneno ambayo tunaweza
kutumia, hata singefikiria kumpa kazi," Bw Trump alisema kumhusu Bw
Bannon.
Kwenye mahojiano yake na New York Times, rais huyo mteule
alizungumzia mambo mengi yakiwemo:
§
Shemeji yake Jared Kushner, mfanyabiashara wa nyumba na makao
ambaye hana ujuzi katika demokrasia, anaweza kusaidia kupatikana kwa amani kati
ya Waisraeli na Wapalestina, alisema. Bw Kushner ni mumewe Ivanka, bintiye Bw
Trump na ni Myahudi.
§
Marekani haifai kuwa "mjenzi wa mataifa" duniani,
alisema.
§
Viongozi wa Republican Paul Ryan na Mitch McConnell
"wanampenda tena, alisema
§
Anaweza kuendesha biashara zake na nchi pia, bila kuwa na
mgongano wa maslahi
§
Kuna uhusiano fulani kati ya shughuli za kibinadamu na mabadiliko
ya tabia nchi
Mapema Jumanne, msemaji wa Bw Trump alisema kiongozi huyo
hatafuatilia sana ahadi yake ya kuanzishwa kwa uchunguzi mpya kuhusu kashfa ya
barua pepe ya aliyekuwa mgombea urais wa chama cha Democratic Hillary Clinton.
Mshauri wake alisema rais huyo mteule hatamteua mwendesha
mashtaka maalum wa kumchunguza Bi Clinton, na kwamba kuachwa kwa suala hilo
kutamsaidia "kupona".
Baadaye, bw Trump alinukuliwa akiambia New York Times:
"Sitaki kuumiza familia ya Clinton, sitaki kamwe.
"Alipitia mengi na ameumia kwa njia nyingi kuu
tofauti."
No comments:
Post a Comment