Hatimaye beki wa klabu ya Simba FC, Mohamed ‘Tshabalala’
Hussein anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na kuanza kupunguza
presha za mashabiki wa timu hiyo waliofikiria kuwa anaondoka.
Akiongea
na Dar 24, Meneja wa mchezaji huyo, Herry Mzozo amesema, “Ninaweza kusema
Tshabalala amebakisha kama asilimi 20, kukamilisha taratibu zote za kuendelea
kuitumikia simba, labda nikuweke wazi kinachoendelea hivi sasa ni masuala ya
kibenki ambayo yatakamilisha huu mchakato.”
“Viongozi wa Simba walikua na
mazungumzo ya muda mrefu na Tshabalala na nikueleze kwamba, hatua hii ilianza
tangu mwanzoni mwa msimu huu na ukaribu uliopo baina ya mchezaji wangu na
uongozi wake ndio umekuwa chachu ya mafanikio ya kusainiwa kwa mkataba wa miaka
miwili,” ameongeza.
“Ninaweza kusema katika suala hili
Yanga walizushiwa, lakini hakuna ukweli wowote kuhusu mipango iliyokua
ikiendelea chini chini kumuhusu Tshabalala, japo kwa upande wangu
ninazichukulia taarifa hizo kama kunogesha mchezo wa soka ambao siku zote
umekua na maneno mengi.”
Awali mchezaji huyo alidaiwa
kuwindwa kwa karibu na timu ya Yanga.
No comments:
Post a Comment