Maafisa wa uchunguzi wa mjini Los Angeles wamesitisha uchunguzi wa madai
yanayomkabili Brad Pitt kwa kuwanyanyasa watoto wake mwezi Septemba mwaka huu
wakati wakiwa kwenye ndege binafsi na familia yake.
Msemaji
wa idara ya watoto na huduma za familia waliokuwa wakichunguza madai hayo na
maafisa wa Los Angeles, amesema idara hiyo haiwezi kuthibitisha iwapo maafisa
wake walimchunguza Pitt.
Kwa sasa Brad anapambana kupata
haki ya kuweza kukaa na watoto huku akiwa ameshatengana na mkewe [Angelina
Jolie] ambaye amefungua kesi ya kudai talaka.
Wawili hao wana watoto sita.
No comments:
Post a Comment