Ushuru mkubwa unaotozwa katika bandari ya Dar es Salaam, umemzuia Baby
Madaha kuingiza vifaa vyake vya filamu alivyovinunua mwaka jana mjini Dubai.
Muimbaji
na muigizaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa serikali ya awamu ya tano imeongeza
ushuru kiasi cha kuharibu mipango ya watu wengi. Amedai kuwa vifaa hivyo bado
vipo Dubai alikohamishia makazi yake.
“Nilileta baadhi ya vitu lakini
nikawa natakiwa nilipe nusu ya price ambayo nimenunulia. Kwa mfano ile mashine
ya dubbing, nimenunua milioni 20 kwahiyo nusu yake ni milioni 10 ninaitoa wapi
kama msanii tu wa kawaida? amehoji Madaha.
Muimbaji huyo amesema anachosuburia kwa sasa ni kuangalia kama kweli
serikali imepanga kuondoa ushuru kwa wasanii kwakuwa wataanza kutozwa kodi.
No comments:
Post a Comment