Mwanamume mwenye miaka 45 Yohana
Omari anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kiume mwenye
umri wa miaka 16, kwa zaidi ya miaka miwili.
Omari ametoroka baada ya kupata
taarifa kuwa anatafutwa na wananchi kutokana na tukio alilokuwa akimfanyia
kijana huyo (jina linahifadhiwa) tangu mwaka 2013.
Akizungumzia tukio hilo, kijana
huyo alisema kuanzia mwaka huo, akiwa darasa la nne amekuwa akifanyiwa kitendo
hicho na baba yake na kukatazwa asiseme.
Alisema siku ya kwanza alipobaini
anafanyiwa ilikuwa usiku akiwa amelala, alishtuka kutokana na kuhisi maumivu
makali na kumkuta baba yake amemlalia juu.
Alifafanua kuwa kuanzia hapo hayo
yakawa ndiyo maisha yake na anapolalamika hukosa baadhi ya huduma, jambo
lililokuwa likimlazimu akubali kuendelea kwa shingo upande.
“Kuna mafuta huwa ananipaka
na kunifanyia kitendo hicho, nimeishi kwa tabu ikiwamo kuamka asubuhi nimechoka
na sina hamu ya jambo lolote, natamani kulala.
“Imefikia mahali natoka majimaji
hadi kuogopa kujichanganya na wenzangu,” alisema kijana
huyo.
Kijana huyo alisema kabla ya kuishi
na baba yake, alikuwa anaishi na mama yake, lakini alipata mwanamume akaolewa
kwa sharti la kutokuishi na yeye, ndipo akampeleka kwa baba yake.
Alieleza kuwa licha ya kuwaeleza
ndugu wa familia, wakiwamo bibi zake, hakuna walichomsaidia.
“Nimemaliza darasa la saba,
nimechaguliwa kujiunga sekondari, lakini sina uhakika wa kuendelea na
masomo.
“Baba amekimbia na kuna viashiria
alitumia rushwa, ulinzi shirikishi badala ya kumkamata walimtorosha,” alisema.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa
Kwa Mustapha Pugu, Dar es Salaam, Bahati Omari alisema baada ya kupata taarifa
hizo, kwa kushirikiana na vijana wake, walifikisha taarifa polisi ili akamatwe
lakini alikuwa ameshatoroka.
Askari polisi mmoja wa eneo hilo
alisema baada ya kupokea malalamiko hayo, walimpeleka hospitali kijana huyo
kumfanyia vipimo ambavyo alibainisha kuwa amefanyiwa kitendo hicho mara
nyingi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,
Salum Hamduni alisema suala hilo lipo chini ya upelelezi.
“Tumepokea hayo malalamiko,
tunayachunguza kwa sababu yanachanganya, amekuwa akifanyiwa vitendo hivyo tangu
mwaka 2013 na amekuja kubainisha leo, hivyo inahitaji upelelezi wa kina,” alisema
Hamduni.
No comments:
Post a Comment