Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Edward Lowassa amesema kuwa aliyekuwa Rais wa Cuba na
mwana mapinduzi wa nchi hiyo, Fidel Castro alimhamasisha kuingia katika
uongozi.
Ameyasema hayo alipotembelea
ubalozi wa Cuba hapa nchini kutoa pole na kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo
cha Castro kilichotokea Novemba 25 mwaka huu jijini Havana nchini Cuba.
Lowassa amesema Marehemu Castro
alikuwa mwana mapinduzi na ni miongoni mwa wanasiasa waliomhamasisha kuingia
kwenye uongozi kutokana na alivyokuwa akiwatetea masikini na wanyonge duniani,
hali ambayo imelisababishia taifa hilo dogo kuogopwa kutokana na uimara wake.
“Castro alikuwa kiongozi imara
sana,kila kiongozi makini lazima awe kinara wa kuwatetea wanyonge na
masikini popote walipo”alisema Lowassa.
Lowassa amesema kuwa Castro
aliifanya Cuba pamoja na udongo wake uitikise dunia kwa kuwa kila mahali ukienda
ni lazima utasikia jina la Castro.
No comments:
Post a Comment