Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema serikali ina mpango
wa kujenga mahakama 20 za mwanzo katika mkoa wake.
Mkuu
wa mkoa huyo amesema hayo alipokutana na waziri wa katika na sheria, Dkt
Harrison Mwakyembe Jumatatu hii jijini humo.
“Mimi na wakuu wangu wa wilaya
tumemuahidi mheshimiwa waziri kwenye mkoa wetu wa Dar es Salaam,tutajenga
mahakama za mwanzo 20 ili kuweka kuongeza kasi ya utoaji na upatikanaji wa haki
kwa wananchi endapo wanapelekwa katika vituo vya polisi kupelekwa mahakamani au
pale ambapo wanakwenda mahakamani baada ya kukaa maamuzi kwa muda mrefu.
Tunategemea kutoka wizarani tutapokea ramani ina muongozo wa vituo viweje na
mahakama ziweje,” amesema Makonda.
Hivi karibuni mkuu huyo wa mkoa
alileta wanasheria 35 katika mkoa wake watakaotoa msaada wa kisheria kwa
wananchi.
BY: EMMY MWAIPOPO
No comments:
Post a Comment