Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo(LGTI), Emanuel
Gibali na wenzake wawili wamepandishwa kizimbani Mahakama ya Wilaya ya Dodoma
kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh 12.4 milioni kutoka Manispaa ya Morogoro.
Akisoma
mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Godfrey Pius, Mwendesha
Mashtaka kutoka Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru), Biswaro
Biswaro alisema washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa manne ambayo waliyafanya
Septemba, 2015 chuoni hapo.
Biswaro aliwataja washtakiwa
wengine kuwa ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Utafiti ,Ushauri na Mafunzo Mafupi,
Benjamen Magori na Mhasibu wa Chuo hicho, Eliakundi Samanya.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo,
Hakimu Pius alisema dhamana zipo wazi na kutoa masharti kuwa kila mmoja anatakiwa
kujidhamini mwenyewe kwa mali isiyohamishika yenye thamani ya zaidi ya Sh 2
milioni na dhamini moja mwenye barua ya utambulisho kutoka serikali za mitaa.
Watuhumiwa wote watatu wapo nje kwa
dhamana baada ya kutimiza msharti ya dhamana na kesi yao itatajwa tena januari
18, waka 2017 .
No comments:
Post a Comment