Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt Harrison Mwakyembe amesema serikali
inatarajia kujadili kushusha kiwango cha fedha kinachohusika katika makosa ya
rushwa na uhujumu uchumi kwenye mahakama ya mafisadi ili kukomesha vitendo vya
rushwa.
Waziri
Mwakyembe alitoa kauli hiyo Jumatatu hii baada ya kufanya mazungumzo na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
“Nimeulizwa sana na waandishi wa
habari tangu Julai hadi sasa walitegemea kungekuwa na kesi nyingi lakini kuna
kesi moja katika Mahakama ya mafisadi tumekuja kubaini kwamba uchache wa kesi
ndiyo mafanikio makubwa ya hatua ya kisheria tuliyochukua,” alisema.
“Sisi kama serikali tukiona wizi
sasa umeanza kupungua na kuenea katika viwango vya shilingi milioni 400, 500,
700 tumeanza kujadiliana kuangalia uwezekano wa kushusha kiwango cha fedha ili
tuweze kukomesha kabisa udokozi, ubadhilifu, wizi wa fedha au mali ya umma,”
aliongeza.
Waziri huyo alishukuru uamuzi wa mkuu
wa mkoa huo, Paul Makonda kutafuta vijana wanaojua sheria ili kusaidia wananchi
kabla ya kwenda mahakamani ni mzuri.
BY: EMMY MWAIPOPO
No comments:
Post a Comment