Urusi imeonya kwamba italipiza
kisasi hatua ya rais wa Marekani Barrack Obama ya kuwatimua wanadiplomaisa 35
wa Urusi kufuatia tuhuma kwamba Urusi iliingilia maswala ya uchaguzi wa
Marekani kwa njia ya udukuzi wa mitandaoni.
Obama amesema Urusi pia imekuwa
ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani.
Kwa upande wake, rais mteule Donald
Trump ambae mara kwa mara amekuwa akizipuuzilia taarifa hizo za udukuzi, sasa
amesema atakutana na wakuu wa kiintellijensia wa Marekani ili kupata undani
zaidi wa swala hilo.
Msemaji wa rais Vladmir Putin
amesema kuwa hatua zitakazochukuliwa na Urusi zitaiathiri Marekani.
Hatahivyo amesema kuwa Urusi
itasubiri hadi rais mteule Donald Trump ambaye amepinga tuhuma hizo za udukuzi
atakapochukua mamlaka.
Urusi imekana madai yoyote ya
udukuzi na kuvitaja vikwazo hivyo vya Marekani kama visivyo na msingi.
Siku ya Alhamisi, Idara ya maswala
ya kigeni nchini Marekani ilitangaza kwamba mabalozi hao 35 kutoka Urusi pamoja
na wasaidizi wao huko San Fransisco hawatakiwi Marekani na kuwapatia wao
na familia zao muda wa saa 72 kuondoka nchi humo.
No comments:
Post a Comment