Goodmorning. Katika uchaguzi huu
mdogo CUF ilikuwa inatetea kata 1 ya Kimwani Muleba na CHADEMA ilikuwa inatetea
kata 1 ya Duru, Babati. Kata zingine zote zilikuwa za CCM na zilikuwa
zinatetewa na CCM.
Matokeo yanaonesha CCM imetetea
viti vyake vyote vya udiwani (takribani 20), CUF imenyang’anywa kiti chake
kimoja (Kimwani) na CHADEMA imelinda kiti chake kimoja (Duru).
Kwa vyovyote vile vyama mbadala
haviwezi kujivunia matokeo haya kwani havikuweza kuishinda CCM, na CCM haina
cha kutambia kwani imeongeza kata moja tu. Kwa sasa nina mambo kadha ya
kuzungumza;
1.
Hali halisi inaonesha kuwa kama vyama mbadala vingeshirikiana
vingelishinda kata si zaidi ya 7 hivi. Bahati mbaya mashirikiano haya
yalikosekana tangu mwanzo baada ya upande wa “CUF ya Msajili na Bwana Yule”
kusisitiza kuwa wataweka wagombea nchi nzima na hakuna UKAWA.
2.
Lakini pia, hata shajihisho la ushirikiano mkubwa zaidi
lililokuja kuzuliwa na kaka yangu Prof. Kitila Mkumbo lilifanywa TOO LATE kwa
lengo la kutafuta sababu ya kujificha baada ya matokeo. Niliwahi kusema,
kiuzoefu vyama haviwezi kuachiana maeneo wiki moja kabla ya siku ya uchaguzi na
kushauri hivyo si kwa nia njema.
3.
Baada ya CUF ya Msajili na Bwana Yule kujipanga kuvuruga
uchaguzi huu na kushusha spirit ya UKAWA, vyama vya NCCR na CHADEMA pia
vilionelea kila kimoja kijipiganie jambo ambalo ni kosa kubwa. Na madhara ya
migawanyiko yote yalijulikana.
4.
Uzoefu unaonesha kuwa, kuishinda CCM kwenye chaguzi ndogo ni
nadra mno. Kuliwahi kuwa na mfululizo wa chaguzi ndogo, Tarime, Busanda,
Tunduru, Mbeya Vijijini n.k. na kote huko CCM ilishinda isipokuwa Tarime na
baadaye Arumeru. Katika chaguzi ndogo CCM hutawanya rasilimali zake nyingi
zikajaa kwenye majimbo au kata hadi POMONI.
5.
Mkakati wa DOLA na CCM kuvitumia baadhi ya vyama au baadhi ya
viongozi kwenye vyama (mamluki) unaelekea kufanikiwa sana. Lakini, sera za
“Self Protectionism” ndani ya vyama mbadala hata kwenye mambo yanayohitaji
ushirikiano wa kitaifa zitaendelea kuvigharimu vyama vyetu.
6.
Good News kwa ACT Wazalendo kwamba huenda ndicho chama
kilichofanikiwa kwenye uchaguzi huu kuliko vyama vyote (CCM inclusive) kwani
pamoja na uchanga wake kimevishinda baadhi ya vyama vikongwe kwenye kata chache
(kwa idadi ya kura na si ushindi wa jumla). Na hiyo ni alert call kwamba ACT is
needed in the UKAWA basket na kwa hiyo ianze ku BEHAVE like a true party wakati
UKAWA pia ikiiandalia mazingira kisaikolojia.
7.
Bado CCM inashinda chaguzi kwa kutumia mifumo ilele; rushwa,
mabavu, hila, wawakilishi wa NEC na NEC yenyewe, uwezo wa uelewa wa wapiga kura
(Mfano. CCM imepeleka uandikishaji wa Bima ya Afya kwa wananchi kata ya Nkome,
wakati wa uchaguzi = Rushwa).
8.
Vyama vya upinzani vinashindwa chaguzi hizi kwa sababu ya kukosa
ushirikiano wa kweli baina ya vyama hivyo, maelezo namba 7 hapo juu na sentensi
ya kwanza ya maelezo yaliyo namba 5 hapo juu.
8.
Kwa hakika, matokeo haya hayana athari zozote za kufaulu kwa
Magufuli katika sera zake au kushindwa kwa Magufuli katika sera zake. Yaani,
CCM ya Magufuli haijawa na ushawishi wa ziada kwa wapiga kura ili kupata
ushindi huu kwenye ngome zake. CCM bado inashinda chaguzi kibabe na kwa mkakati
dola zaidi bila kujali nani yuko madarakani.
9.
Sijaona connection yoyote kati ya matokeo haya na siasa za 2020.
Vyama vyote vinayo fursa ya kuendelea kujipanga na kama tutafanikiwa kuuvunja
mfumo dola unaoathiri vyombo vya uchaguzi na uhuru wake, unaoondoa mazingira
sawa kwa vyama kufanya siasa n.k, mabadiliko ya kikatiba kwenye NEC na sheria
za uchaguzi na mengine mengi, siasa za 2020 zitakuwa mbichi sana.
Na. Julius S. Mtatiro
No comments:
Post a Comment