Afisa wake wa mawasiliano Sean Spicer amesema hatua hiyo ya rais
inaonesha kwamba "anataka kuwatetea Wamarekani wote, wakiwemo wale ambao
hawajazaliwa."
Agizo hilo ambalo kirasmi
linafahamika kama "the Mexico City Policy" (Sera ya
Jiji la Mexico) huenda likayakera makundi ya kutetea uhuru wa wanawake kuamua
kuhusu uzazi, ambayo tayari yametiwa wasiwasi na msimamo wake wa kupinga utoaji
mimba.
Bw Trump anaunga mkono utoaji mimba upigwe marufuku Marekani.
Lakini hii si mara ya kwanza kwa marufuku dhidi ya ufadhili wa
mashirika ya utoaji mimba nje ya Marekani kutolewa.
Rais wa Republican Ronald Reagan mara ya kwanza alianzisha Sera
ya Jiji la Mexico mwaka 1984 na kuwa wa kwanza kupiga marufuku ufadhili huo.
Lakini chama cha Democratic kilibatilisha marufuku hiyo chini ya
utawala wa Bill Clinton.
Sera hiyo inayataka mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo
yanapokea ufadhili wa serikali ya Marekani kukubali "kutotekeleza na
kutoendeleza au kutohamasisha watu watumie utoaji mimba kama njia ya uzazi wa
mpango katika nchi nyingine".
Kwa miongo mingi, imekuwa kwamba pesa za Marekani haziwezi
kutumiwa katika utoaji mimba katika mataifa ya nje.
Lakini Sera ya Jiji la Mexico inaenda hatua zaidi.
Mwaka 2009, Barack Obama alisitisha utekelezaji wa sera hiyo,
ambayo ilikuwa imrejeshwa chini ya utawala wa Rais George Bush.
Makundi ya kutetea uhuru wa wanawake kuamua kuhusu uzazi
wamepinga hatua hiyo ya Bw Trump.
"Ni jambo la kusikitisha sana kwamba moja ya hatua za
kwanza za Trump inaunganisha mambo mawili kwa pamoja: kunyamazisha wote
wanaotofautiana naye na kuwakandamiza wanawake," taarifa kutoka kwa kundi
la Naral Pro-Choice America imesema.
"Siku mbili baada ya maandamano ya kihistoria ya wanawake
ya kumpinga Trump kufanyika na siku moja baada ya maadhimisho ya uamuzi wa
kihistoria wa mahakama kesi ya Roe v. Wade, Donald Trump anapatia kipaumbele
hatua ya kurejesha ... sera ambayo inawanyamazisha wahudumu wa afya na kuweka
hatarini wagonjwa."
Wakati wa kampeni, Bw Donald Trump, ambaye awali alitetea uhuru
wa wanawake kuamua kuhusu uzazi, aliambia MSNBC kwamba "lazima kuwe na
aina fulani ya adhabu kwa mwanamke" iwapo utoaji mimba utakuwa marufuku.
Baadaye, aliondoa tamko hilo baada ya kushutumiwa vikali na
makundi ya kutetea haki za wanawake.
Maafisa wa kampeni wa Bw Trump walisema waliamini uamuzi
kuhusu uhalali wa utoaji mimba unafaa kuachiwa majimbo yenyewe, na kwamba
adhabu inafaa kutolewa kwa wanaotoa huduma za utoaji mimba.
Alisema anaunga mkono marufuku ya
utoaji mimba ila tu wakati mimba imetokana na "ubakaji, kujamiiana kwa
maharimu au wakati maisha ya mama yamo hatarini".
Bw Trump pia ameahidi kujaza nafasi
ya jaji iliyo wazi Mahakama ya Juu na jaji ambaye ni mhafidhina kuhusu masuala
ya kijamii.
Hayo yakijiri, Bunge la Congress
limeashiria nia yake ya kuondoa ufadhili wa serikali kwa kundi la Planned
Parenthood, kundi linalotoa huduma za afya ya uzazi Marekani na nje ya taifa
hilo.
No comments:
Post a Comment