Mahakama ya Rufaa nchini Marekani
imekataa kuirudisha tena marufuku iliyowekwa na Rais Donald Trump ya wasafiri
kutoka nchi saba za kiislamu na Wakimbizi wote kuingia nchini humo.
Jopo la Majaji watatu kwa kauli moja limekataa kuupindua uamuzi
uliotolewa na Jaji kutoka mji wa Seattle, ambaye wiki iliyopita alizizuia
sehemu za amri iliyotolewa na Rais huyo wa Marekani.
Habari zinasema kwamba uamuzi huo kwa sasa utapelekwa katika
Mahakama ya juu.
Na muda mfupi tu baada ya Uamuzi huo wa mahakama kutangazwa,
Rais Donald Trum aliwaambia waandishi wa habari kwamba ana uhakika mwisho wake
ataibuka mshindi.
''Ni uamuzi wa kisiasa na tutaenda kukutana mahakamani. Na
natarajia kufanya hivyo, Tuna hali ambayo usalama wa nchi yetu uko hatarini na
ni hali mbaya sana..'' Alisema Trump.
Katika hatua nyingine tena Rais Trump ametangaza
mfululizo wa amri za Rais kwa lengo la kupunguza uhalifu. Akizungumza wakati
wav kuapishwa kwa Mwanasheria mkuu wa nchi hiyo, Rais wa Marekani amesema
uhalifu umeongezeka nchini Marekani na utawala wake utalishughulikia suala hilo
kuamzia sasa.
Amri hizo zilizotangazwa ni pamoja
na kukabiliana na magenge ya madawa ya kulevya na wafanyabiashara za kihalifu.
No comments:
Post a Comment