Hospitali moja nchini Uchina imekiri
kwamba watu watano waliambukizwa virusi vinavyosababisha Ukimwi hospitalini
humo kimakosa.
Waliambukizwa na mhudumu wa afya ambaye alitumia tena vifaa vya
matibabu ambavyo vilifaa kutupwa baada ya kutumiwa.
Maafisa wanasema mhudumu huyo alitumia bomba lililotumiwa
kumtibu mgonjwa mwenye Ukimwi kwa wagonjwa wengine.
Maafisa wa utawala wa mkoa wametaja kisa hicho kama
"ukiukaji mkubwa wa utaratibu".
Tayari wahudumu watano wamefutwa kazi katika hospitali hiyo ya
mkoa ya Zhejiang katika mkoa wa Hangzhou.
Maafisa hao wa afya wa mkoa wamesema walifahamishwa kuhusu kisa
hicho 26 Januari.
Lakini kwenye taarifa, hawajasema iwapo kuna wagonjwa wengine
ambao huenda waliwekwa kwenye hatari ya kuambukizwa na ni maradhi ya aina gani
wale walioambukizwa walikuwa wakitibiwa.
Wale walioambukizwa watapokea matibabu na fidia, taarifa fupi
ilisema.
Katika ripoti ya hivi karibuni, China ilisema kulikuwa na watu
501,000 waliokuwa wameambukizwa virusi vya Ukimwi kufikia mwaka 2014.
No comments:
Post a Comment