Wakati akianza kuhutubia alikatizwa
na kelele za Wabunge wa upinzani, waliokuwa wakimkosoa.
Miongoni mwa ukosoaji dhidi yake
kuhusiana na matatizo ya kiuchumi na rushwa, ulifanywa pia na baadhi ya wabunge
kutoka chama tawala.
Awali nje ya bunge la nchi hiyo,
Polisi walifyatua mabomu kuwashtua watu waliokuwa wakifanya vurugu, ili kuweza
kuwasambaratisha.
Rais Jacob Zuma alipeleka kikosi
cha wanajeshi zaidi ya elfu nne bungeni hapo ili kulinda usalama, wakati akitoa
hutuba yake.
No comments:
Post a Comment