Mtu mmoja amefariki dunia baada ya kuzama katika bwawa la maji lililopo mtaa wa njia panda katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na mkoani Geita.
Tukio hilo limetokea
mapema hapo jana majira ya saa kumi na moja jioni ambapo mtu
huyo alikuwa akioga katika bwawa hilo akiwa na wenzake baada ya mda
mfupi alipotea ghafra kutokana na bwawa hilo kuwa na kina kirefu ndipo baadhi ya wakazi katika eneo hilo walipo jitokeza na kujaribu kumtafuta ndani ya bwawa
hilo lakini hawakufanikiwa kumuona , ndipo shughuli za kumtafuta mtu huyo
zimeendelea tena mapema hii leo na mnamo
majira ya saa sita mchana mwili wa marehemu huyo umefanikiwa kuonekana .
Mwenyekiti wa mtaa huo bw
michael chuma amemtaja alie fariki dunia kuwa ni kamugisha budodi mwenye
umri wa miaka 14 mkazi wa kijiji cha mapinduzi wilayani chato na alikuwa
mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi mapinduzi .
Bw chuma amewata wazazi na walezi katika mamlaka ya mji mdogo
wa katoro kuto waruhusu watoto
wenye umri mdogo
kuchota maji wala kuoga katika
eneo hilo kutokana na bwawa hilo kuwa na kina kirefu pamoja na toze nzito kitu
ambacho kina kuwa hatarishi kwa watoto hao.
Aidha baadhi ya wakazi katika eneo hilo bw manyindo pamoja na victoria
msakila wameiomba serikali ya mtaa huo kuweka uzio katika eneo hilo kwa
lengo la kuzuia watoto wenye umri mdogo
kuto tumia bwawa hilo.
No comments:
Post a Comment