Mchungaji Josephat Gwajima ni mmoja wa watu waliotengeneza vichwa vya
habari wiki hii baada ya kutajwa kwenye orodha ya pili ya mkuu wa mkoa wa Dar
es Salaam ya watu wanaotuhumiwa kuhusika kwenye biashara ya madawa ya kulevya.
Gwajima
anafahamika kwa utajiri mkubwa kiasi cha kumiliki ndege, helikopta na kudai
kuwa na mpango wa kununua treni. Utajiri wake umekuwa ukizusha maswali mengi na
kupitia mkutano wake na waandishi wa habari Alhamis hii uliofanyika kanisani
kwake, Gwajima alielezea vyanzo vyake vingine vya mapato.
“Cha kwanza mimi ni daktari wa
philosophy, ni lecturer peke yake Tanzania kwa malecturer wa kidini ambaye
husafiri kwenda kulecture nje ya nchi,” alisema.
“Lecture yangu moja nalipwa dola
elfu moja, ambayo ni sawa sawa na milioni 2 na laki kama nne, moja ya saa moja.
Nikienda kulecture Japan naweza kulecture miezi mitatu na mimi sijawahi
kusafiri na hela mfukoni, hela zote zinakuja kwa benki mpaka hapa. Chini ya
kanisa letu kuna kampuni zinaitwa Mahanai Organisations, ni makampuni makubwa.”
Gwajima ametii agizo la kwenda
kuhojiwa kwenye kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment