Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt
Harrison Mwakyembe jana alisema kuwa atakifuta Chama cha Wanasheria Tanganyika
(Tanganyika Law Society (TLS)) kwa madai kuwa kimesahau misingi yake na kuanza
kufanya kazi kama chama cha siasa.
Waziri Mwakyembe alisema kuwa, kama
wanataka kufanykazi kama chama cha siasa, basi yeye ataongea na msajili wa
vyama vya siasa nchini ili cha hicho kipya kisajiliwe.
Kufuatia kauli hiyo, Mwanasheria
Mkuu wa CHADEMA, Mbunge wa Singida Mashariki na mgombea Urais wa TLS, Tundu
Lissu ameandika waraka huu kwenda kwa wanasheria wenzake.
Mawakili wenzangu. Mimi binafsi
sijashangazwa na kauli ya Dkt. Mwakyembe kwamba ataifuta TLS kama itajiingiza
katika harakati za kisiasa. Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa serikali ya
Tanzania kutoa vitisho vya kuifuta TLS.
Waziri Mkuu hayati Edward Sokoine
aliwahi kutishia hivyo katika kilele cha vita dhidi ya wahujumu uchumi miaka ya
mwanzo ya ’80. Na hata kabla ya hapo katika miaka ya ’60 na ’70 watangulizi wa
Sokoine walijaribu kufanya hivyo hivyo. In fact, kuanzishwa kwa Tanzania Legal
Corporation kipindi hicho kulikuwa driven in part na jitihada za kuondoa the
private bar.
Vitisho dhidi ya TLS vilirudi miaka
ya ’90 wakati wa Lyatonga Mrema. Kitu kimoja kiko common katika vitisho hivyo
vyote. Vitisho hivi vimetolewa kila wakati TLS na private bar wanapo-assert
their independence na wanapoanza kutetea utawala wa sheria na kupinga state
lawlessness and impunity of the rulers.
Mawakili wakiwa kimya na TLS ikiwa
mfukoni mwa serikali na wasipohoji matumizi mabaya ya madaraka basi wanakuwa
darlings wa serikali.
Kuna kitu kingine ambacho ni common
katika vitisho hivi. Havijawahi kufanikiwa na havitafanikiwa. Sheikh Abeid
Amani Karume alipiga marufuku private legal practice mara baada ya Mapinduzi ya
Zanzibar ya ’64. Tanzania ya leo sio Zanzibar ya miaka ya ’60 na ’70,
hatutakubali udikteta wa aina ya Karume au wa aina nyingine yoyote kwenye
Tanzania ya leo.
Inaelekea Dkt. Mwakyembe hafahamu
au anajisahaulisha jinsi ambavyo TLS na mawakili binafsi walivyo embedded
kwenye mfumo wetu wa kikatiba na kisheria. Simply put, ukifuta TLS maana yake
ni kwamba hakuna wakili binafsi hata mmoja nchi nzima. Mfumo mzima wa
kimahakama unategemea uwepo wa mawakili na kwa hiyo uwepo wa TLS. Mahakama
karibu zote zitashindwa kufanya kazi kusipokuwa na mawakili binafsi. The same
applies to various tribunals and other judicial and quasi judicial bodies.
Aidha, kuna taasisi nyingi
zilizoundwa na Katiba yetu kama vile Judicial Service Commission na Law Reform
Commission ambazo zinakuwa properly constituted kukiwa na uwakilishi wa TLS.
Kuna taasisi nyingine nyingi ambazo zimeanzishwa na sheria za kawaida ambazo
composition yake inakamilika kukiwa na representation ya TLS. Hiyo legal,
constitutional and political upheaval itakayotokana na kufutwa kwa TLS will be
unprecedented and unimaginable kwa mtu mwenye akili timamu.
Dkt. Mwakyembe ana akili timamu. He
must be joking. Hawezi kufuta TLS. Anachotaka kufanya ni kuwatisha mawakili ili
wachague watu wale wale wa miaka yote kuongoza TLS. Anatutisha ili tuendelee na
status quo katika uongozi wa TLS. Hataki tufanye mabadiliko yanayohitajika ili
TLS yetu isichukue nafasi yake stahiki katika kuamua mustakbala wa nchi yetu na
wa taaluma yetu.
Nawataka viongozi na wanachama wa
TLS wamkemee Dkt. Mwakyembe in the strongest possible terms. Nawataka wagombea
wenzangu wa nafasi mbali mbali za uongozi katika TLS wajitokeze hadharani na
kulaani kauli ya Dkt. Mwakyembe in no uncertain terms. Wakinyamaza tutawajua
wako upande wa nani: status quo au mabadiliko. And I’ll ask you all to vote
accordingly.
Tundu Lissu.
No comments:
Post a Comment