Wimbo mpya wa rapper Nikki Mbishi,
I’m Sorry JK umefungiwa.
Uamuzi huo umekuja saa chache baada
ya rapper huyo kuitwa na Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA Jumatano hii
kujielezea kuhusiana na wimbo huo. Kupitia Instagram, Nikki amewaonya watu
dhidi ya kuusambaza wimbo huo kwakuwa mkono wa sheria utawaangukia.
“Naomba niombe radhi kwa vyombo
vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa
“I’M SORRY JK” uliositishwa na hii ni kwa usalama wao na wangu pia,” ameandika kwenye
Instagram.
“Napokea simu nyingi sana
zikihitaji maelezo juu ya suala hilo ila kiukweli kwa watakaohitaji taarifa
kamili wanaweza kufika ofisi za BASATA,naomba nisiwe msemaji tena juu ya jambo
hili,” ameongeza.
Pia ameonya, “Kwa yeyote
atakayeendelea kuusambaza au kuucheza popote pale mimi sitohusika naye maana technology
iko huru popote duniani na siwezi kuzuia watu wasiupate kwa kuwa
ushasambaa,hivyo chukua tahadhari ili usijikute mikononi mwa sheria. Asanteni
sana,naomba msubiri ujio wangu mpya wa #SINGELI na aina nyingine za muziki kama
#NAIJA #MCHIRIKU n.k.”
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe
ameandika kwenye Facebook:Serikali imepiga marufuku wimbo wa msanii Nikki
Mbishi. Wallah nilidhani ni utani kumbe Kweli? Serikali hii inachoogopa ni
nini? Dah kua uyaone.”
No comments:
Post a Comment