Mkuu wa wilaya ya geita mkoani geita mwalimu
hermani kapufi ameahidi kuwashughulikia kikamilifu wanaume wenye tabia ya
kuwaterekeza wake zao wenye ujauzipo badala ya kuwapatia msaada wa kuwapeleka
katika vituo vya afya kwa ajiri ya vipimo kabla ya kujifungua.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa idadi kubwa ya
vifo vya akina mama wajawazito pamoja na watoto wilayani geita kutokana baadhi ya kina mama kutohudhulia
kriniki wakati wa ujauzito wao.
Akizungumza na wananchi katika kituo cha afya cha katoro
mwalimu kapufi amewataka viongozi katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro ikiwa ni pamoja na watedaji wa kata na vijiji
kutoa elimu kwa kina mama wajawazito kutambua umuhimu wa kujifungulia katika
vituo vya afya.
Kapufi
amesema kwa wanaume ambao hawatambui umuhimu wa mwanamke
mjamzito kuhudhulia katika kituo cha
afya, atapambana nao kikamilifu ili kuhakikisha suala hilo linaonekana kuwa la
muhimu katika jamii .
Hata hivyo mbunge wa jimbo la busanda mheshimiwa lolencia bukwiba ametumia fursa hiyo kuwa omba kina mama wajawazito kuhudhulia na kuzingatia ratiba ya clinic ili
kuepuka madhara ambayo yanaweza kujitokeza
wakati wa kujifungua.
No comments:
Post a Comment