Serikali mkoani geita imesema haita walipa fidia
wananchi watakao bomolewa nyumba zao au kukatiwa miti pindi zoezi la usambazaji wa nguzo za umeme
vijijini litakapo kuwa limeanza kutekelezwa.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa
maeneo mengi wilayani geita ambayo
hayajapatiwa umeme kutokana na miundo mbinu kuwa duni ikiwa ni pamoja na ujenzi
wa nyumba za makazi kiholela jambo
ambalo limesababisha shirika la umeme tanzania (tanesco) kushindwa kupitisha
nguzo kwasababu hiyo.
Akizungumza na wananchi katika mamlaka
ya mji mdogo wa katoro mkuu wa wilaya ya
geita mwalimu hermani kapufi amesema kuwa serikali itapeleka nguzo
maeneo ambayo hayajapatiwa umeme kutokana na hilo hakuna mwananchi atakae lipwa
fidia kama nyumba au miti yake itakuwa kandokando ya ramani ambapo nguzo za
umeme zinatarajia kupita katika maeneo hayo.
Mwalimu kapufi amewataka wananchi walio tandaza
nyaya katika nyumba zao wategemee kufungiwa umeme mwezi wa tatu na wanne na kwa
wale ambao hawaja tandaza nyaya katika nyumba zao waweke ili zoezi hilo
lifanyike kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment