Mcheza
tenesi Petra Kvitova ambae alivamiwa mwezi Desemba mwaka jana na kukatwa na
kisu mkononi ameweza kuanza kushika raketi ya kuchezea tenesi .
Lakini hata
hivyo Kvitova hajui ni lini atarejea tena uwanja kuweza kucheza mchezo huo ,
tangu awali madaktari walisema itamchukua miezi sita kwa nyota huyo kuweza
kurejea tena uwanjani.
Msemaji wa
mchezaji huyo Karel Tejkal, amesema"Preta anaendelea vizuri na mkono wake
unapona kama ilivyotarajiwa,"
Kwa sasa
mchezaji huyo anaweza kuutumia mkono wake kama kawaida katika shughuli zake za
kila siku na amekua akifanya mazoezi katika visiwa vya Canary
No comments:
Post a Comment