Afisa mkuu wa
jeshi la Israel ameongeza uzito katika vyombo vya habari vya Kiarabu kwamba
kundi la wapiganaji wa Hezbollah lilihusika katika mauaji ya kamanda wake
nchini Syria 2016.
Luteni jenerali
Gadi Eisenkot alisema kuwa idara ya ujasusi ya Israel pia ilibaini kwamba
Mustafa Amine Badreddine aliuliwa na wapiganaji wake.
Aliuawa katika
mlipuko karibu na Damscus ambapo kundi la wapiganaji la madhehebu ya kishia
lililaumu wapiganaji wenye itikadi kali wa Sunni.
Badreddine
aliaminika kuendesha operesheni zake nchini Syria tangu 2011.
Ndege za Israeli
zashambulia Syria
Vikwazo kwa
Makamu wa Rais Venezuela
Wanamgambo wa
Shia walenga kuukomboa mji wa Tal Afar,
Hezbollah
linahusishwa pakubwa katika vita vya wenye kwa wenyewe nchini humo, likiwa
limesambaza maelfu ya wapiganaji ili kumuunga mkono rais Bashar al-Asaad.
Mapema mwezi huu,
kituo cha habari cha al-Arabia kilisema kuwa uchunguzi wake mwezi huu kuhusu
mauji ya Bedraddine ulibaini kwamba kamanda huyo aliuawa kutokana na agizo la
Hassan Nasrallah.
Ripoti hiyo
inasema kuwa Hassan Nasrallah alishinikizwa kumuua Bedraddine na meja jenerali
Qasema Soleiman,kiongozi wa walinzi wa jeshi la Iran.
No comments:
Post a Comment