Watu nchini
Mexico wameelezea ghadhabu zao baada ya picha ya mtaalii mmoja kuchapishwa
kwenye mitandao ya kijamii akiwa ameshika bunduki ya afisa wa polisi.
Mtalii huyo
anayetabasamu na ambaye hana shati anaonekana akiwa na polisi wawili
waliosimama kando katika eneo la starere la Playa del Carmen.
Vyombo vya
habari vilisema kuwa bunduki hiyo haikuwa na risasi.
Hata hivyo
ni kinyume na sheria afisa wa polisi kusalimisha bunduki yake.
Jumla ya
polisi 80 walitumwa eneo hilo hivi majuzi kukabiliana na visa vya uhalifu.
Mwezi
Januari watu watano waliuawa eneo la Playa del Carmen, wakati mwanamume mmoja
alifyatua risasi kwa klabu moja ya usiku wakati wa tamasha moja maarufu ya muziki,
No comments:
Post a Comment