Kocha wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amewajibu mashabiki wa
Chelsea waliokuwa wakimuita ‘Yuda’ katika mechi ya Kombe la FA robo fainali
dhidi ya Chelsea.
Sehemu
moja ya mashabiki ilipiga kelele “F*** off Mourinho”, “Wewe si Special tena” na
“ni Yuda” wakimaanisha msaliti katika ushindi wa Chelsea wa 1-0 katika uwanja
wa Stamford Bridge.
Katika mahojiano na waandishi wa
habari baada ya mechi hiyo Mourinho alijibu.
“Wanaweza kuniita chochote
wapendacho. Hadi watakapopata meneja anayewashindia mataji manne ya Ligi ya
Uingereza, Mimi ni nambari moja,” alisema Mourinho ambaye alitupiwa virago
Chelsea msimu uliopita.
Katika vipindi viwili tofauti kama
meneja wa Chelsea (2004-2007 na 2013-2015), Mourinho aliinoa Chelsea na kuipa
mataji manne ya ligi, moja la FA na matatu ya Kombe la Ligi.
“Watakapopata mtu wa kuwapa mataji
manne ya Ligi ya Uingereza, basi nitakuwa namba mbili. Lakini hadi sasa Yuda
bado ni namba moja.”
No comments:
Post a Comment