Baada ya kushikiliwa na polisi kwa takriban siku 4, Vanessa Mdee
ameachiwa kwa dhamana Jumatatu hii.
Vanessa
ambaye alishikiliwa muda mfupi baada ya kurejea kutoka Afrika Kusini ni
miongoni mwa mastaa waliotajwa kwenye orodha ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam,
Paul Makonda kutokana kuhusishwa na matumizi na biashara ya dawa za kulevya.
Inadaiwa kuwa Vee anatetewa na
mwanasheria maarufu, Peter Kibatala.
Watu wengi wakiwemo mastaa nchini
walikuwa wakimtetea kutaka kuachiwa huru kutokana na kile wanachoamini kuwa
anaonewa.
No comments:
Post a Comment