Bondia kutoka nchini Uingereza Amir Khan hatopigana tena na bingwa wa
uzani wa Welterweight Manny Pacquiao mwezi ujao kulingana na promota Bob Arum.
Mabondia
hao wawili walikuwa wametangaza pigano hilo kufanyika mnamo mwezi Aprili 28
katika mtandao wa Twitter mwisho wa mwezi Februari huku UAE ikitajwa kuwa eneo
la pigano hilo.
Lakini Arum ameambia ESPN: Pigano
hilo limefutiliwa mbali.
”Ninazungumzia kuhusu pendekezo
jingine lakini sio Khan. Khan hatakuwa tena mpinzani wa Manny”.
Pigano hilo la mwezi Aprili
lilipangwa baada ya mashabiki wa Paqcuiao katika mtandao wa Twitter kumpigia
kura Khan kuwa mpinzani ambaye wangependelea bondia huyo mwenye umri wa miaka
38 kupigana naye.
Khan ambaye mwenye umri wa miaka 30
aliyeshinda medali ya fedha katika uzani wa Lightweight katika michezo ya
Olimpiki ya 2004, alimshinda Kell Brook, raia wa Australia Jeff Horn na
Mmarekani Terence Crawford kwa asilimia 48 ya kura hizo zilizofanywa na
Pacquiao.
Source: BBC
No comments:
Post a Comment