Baadhi ya wanafunzi katika
mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na mkoani geita
wameiomba serikali kuwa chukulia hatua kari za kisheria baadhi ya wazazi na
walezi wenye tabia ya kuwashawishi watoto wa kike wenye umri chini ya miaka 18 kuolewa badala ya kuwa shuleni.
Hatua hiyo imekuja baada ya
shirika la plan internation pamoja
na nelco yanayo jihusisha na haki
za binadamu mkoani geita kuzindua
mradi maalumu wa kupambana na janga la ndoa za utotoni katika
kata tatu zinazo unda mamlaka ya
mji mdogo wa katoro ambazo ni katoro
,ludete pamoja na nyamigota, ambapo
mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miaka
mitatu katika maeneo hayo huku mradi huo ukiongozwa na kaulimbiu isemayo niwajibu wetu wanajamii kumlinda msichana
dhidi ya ndoa za utotoni.
Wanafunzi katika shule ya
sekondari katoro ambapo mradi huo umezinduliwa katika viwanja hivyo wamesema
kuwa wanaiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria baadhi ya wazazi
na walezi wenye tabia ya kuwashawishi watoto wenye umri mdogo kuingia
katika ndoa.
Kwa upande wake afisa
elimu wa wilaya ya geita bw george opiyo ambae alikuwa mgeni
rasimi katika uzinduzi wa mradi huo amesema kuwa serikali haita sita kuwa
chukulia hatua kali za kisheria baadhi
ya wazazi na walezi wenye tabia ya kuwa
ozesha watoto wao badala ya kuwasaidia
kupata elimu ambayo inaweza kuwasaidia katika
maisha yao ya baadae.
Bw george amewataka watoto wakike
wajilinde na kuepuka vishawishi kutokana
na kuwepo kwa baadhi ya wazazi au walezi wanao walazimisha kuolewa jambo mabalo
siyo la kiungwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18 kwani kwa kufanya hivyo
kunaweza kusababisha kifo kwa mtoto wakati wa kujifungua kutokana na kubeba ujauzito huku akiwa na
umri ambao hapaswi kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment