Wananchi katika mamlaka ya
mji mdogo wa Katoro wilayani na mkoani Geita
wameiomba serikali kupiga marufuku uuzaji wa silaha za jadi kiholela ili
kuepuka madhara yanayo weza kujitokeza katika jamii kutokana na silaha hizo
kuuzwa pasipo kufuata utaratibu.
Baadhi ya wananchi hao
wamesema kuwa kumekuwepo na idadi kubwa ya watu katika eneo hilo ambao
wanajishughulisha na biashara hiyo ya
uzaji wa silaha za jadi kiholela jambo ambalo linahatarisha usalama wa watu
kutokana na silaha hizo kufikia hatua ya
kupangwa kandokando ya barabara na
kwenye mirundikano mikubwa ya watu ikiwa
ni pamoja na kwenye viwanja vya michezo.
Wananchi hao wamezitaja silaha zinazo uzwa katika maeneo hayo ni pamoja na Mikuki , Mishale, Visu,Shoka, Sime
pamoja na Mapanga.
Kwa upande wao wafanya
biashara wa silaha hizo Bw,Masalu Rukasi
na Gervas Manyilizu wameeleza kuwa
kabla ya kuingiza sokoni zana hizo kwa ajiri ya biashara wanakuwa na kibari kutoka kwa kiongozi wa
eneo husika kwa sababu ya usalama zaidi .
Wafanyabiashara hao
wamesema kumekuwepo na baadhi ya watu
wanao kiuka taratibu hizo ambazo
wanatakiwa kufuata na badala yake huuza
zana hizo Kihole kitendo ambacho kinahatarisha usalama wa raia katika jamii .
Aidha mwenyekiti wa mamlaka
ya mji mdogo wa katoro Bw Japheti Madoshi amewataka wanao jishughulisha na biashara hiyo kandokando ya
barabara na kwenye mirundikano mikubwa ya watu waache mara moja na badala yake watafute sehemu iliyo salama
kwa ajiri ya biashara hiyo ikiwa ni pamoja na kujenga vibanda vya kuhifadhia
zana hizo.
No comments:
Post a Comment