Mkuu wa utumishi Jeshi la Wananchi Tanazania (JWTZ), Meja
Jenerali Harrison Masebo amekanusha taarifa zinazoenea mitandaoni
kuhusu kutangazwa kwa nafasi za ajira na kwamba watu wanaotangaza hivyo ni
matapeli waepukwe.
Meja Jenerali Masebo amebainisha hayo baada ya kuenea uvumi
mitandaoni na mitaani kwa baadhi ya watu kujifanya wanahusika na jeshi hilo
katika idara ya kutoa ajira kwa wananchi.
"Kumekuwa na vikundi ama watu ambao kwa namna moja ama
nyingine wamekuwa wakijitangaza wao wanauwezo kutoa ajira, vikundi hivyo
msivisikilize siyo vikundi rasmi ama watu hao siyo rasmi kwa niaba ya Mkuu wa
Majeshi nasema kuanzia leo mtu akisiikia kuna mtu anamfuata anamwambia kuna
nafasi ya kujiunga na mafunzo ya JKT ajue huyo mtu siyo halali ni muongo na
tapeli" -alisema Meja Jenerali
Masebo.
Pamoja na Hayo Meja Jenerali Masebo amesema mara zote Jeshi
limekuwa likitoa ufafanuzi kuhusiana na masuala ya ajira lakini wanashangazwa
na kundi hilo namna wanavyofanya kutaka kupitia 'shortcut'.
"Jeshi limekuwa likifafanua mara kwa mara kuhusu taratibu
za kujiunga nafasi za mafunzo JKT na taratibu za kujiunga na jeshi la wananchi
lakini katika mazingira ambayo tunashindwa kuyaelewa hawa watu au vikundi ndiyo
wamekuwa wajanja kiasi cha kuwarubuni vijana, wazazi na wazazi wakaamini kwamba
zipo njia mbadala za kujiunga 'shortcut' napenda kusema hakuna shortcut
hapa" - alisisitiza
Meja Jenerali Masebo
Pamoja na hayo, Meja Jenerali Masebo aliendelea kufafanua baadhi
ya mambo kwa kusema "Kwa vyombo vyote vya ulinzi na usalama hata
wakiwa Uhamiaji, Zima moto, Magereza, Polisi, TANAPA na Jeshi lenyewe ukitaka
kujiunga na Jeshi la Wananchi maana yake ni kwamba kuna utaratibu maalumu
ambapo kwanza kuna kikao ambacho wenyekiti wa kikao hicho ni mimi Mkuu wa
Utumishi Jeshini kwa hiyo vyombo vingine vya ulinzi na usalama vinaleta
wawakilishi ambao ni maofisa watumishi tunakaa pamoja kila taasisi, wanaleta
idadi ya watu wanaowahitaji" - Meja Jenerali Masebo aliongeza.
No comments:
Post a Comment