CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA - TLS CHAKUSANYA MAMILIONI YA FEDHA KWA AJILI YA MATIBABU YA LISSU - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday 12 January 2018

CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA - TLS CHAKUSANYA MAMILIONI YA FEDHA KWA AJILI YA MATIBABU YA LISSU

Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kimesema kimefanikiwa kukusanya Sh138 milioni kugharamia matibabu ya Rais wa Chama hicho, Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven nchini Ubelgiji.

Taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa TLS, Godwin Ngwilimi amesema kiasi hicho wamekipata kutoka kwa watu mbalimbali walijitolea kuchangia wa ndani na nje ya nchi wakiwemo wanachama wa chama hicho.
Kuhusu mchanganuo wa fedha hizo, Ngwilimi amesema kimetumika kulipa gharama za matibabu ya Lissu katika Hospitali ya Nairobi, Leuven na visa kwa watu watatu wakiwa nchini Ubelgiji

Ngwilimi ametoa shukuran kwa wale wote waliojitokeza kuchangia matibabu ya Lissu ambaye pia ni mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa Chadema

Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa katika makazi yake mjini Dodoma ambapo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na usiku wa siku hiyo alihamishiwa Hospitali ya Nairobi alikolazwa hadi Januari 6 baada ya kahamishiwa Leaven, Ubelgiji kwa mazoezi ya viungo na saikolojia.

Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here