MVUA YAUA WATOTO WAWILI WAKITOKA SOKONI - OREST NGOWI

Breaking

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Friday 12 January 2018

MVUA YAUA WATOTO WAWILI WAKITOKA SOKONI

Mvua kubwa iliyonyesha katika kijiji cha Mwekako kata ya Kasenga wilayani Chato mkoani Geita imesababisha vifo vya watoto wawili na kuharibu mali.

Diwani wa Kata ya Kasenga, Damian Vilarie amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema mvua imesababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara. 

Amesema mvua hiyo iliyonyesha kwa saa tatu jana Alhamisi Januari 11 ilisababisha mafuriko yaliyowasomba watoto wawili wa mzee Kurwa waliotoka soko la Igalula kununua bidhaa za nyumbani.

Amesema watoto hao mmoja anakadiriwa kuwa na miaka 13 na mdogo miaka mawili.
Na Rehema Matowo, Mwananchi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Responsive Ads Here