
Mkali wa muziki
anayefanya vizuri na wimbo ‘Salome’ Diamond Platnumz Alhamisi hii siku moja
kabla ya birthday ya mama watoto wake Zari, ameonyesha nyumba ya familia
aliyonunua Afrika Kusini.
Muimbaji huyo
ambaye ni mmoja kati ya wasanii wachache wenye mafanikio makubwa hapa nchini,
hakuweka wazi nyumba hiyo imegharimu kiasi gani kuinunua.
“Wanakazana
kujisifu matajiri ilhali watoto zao wanaishi kwenye Nyumba zakupanga. Halafu
leo yule yule wanaemtukana kutwa kwenye mitandao kuwa masikini, kajawa na
shida, Kanunua nyumba kulekule kwao ili watoto wao waishi maisha bora kama
wanayoyatamani. Heri ya siku ya Kuzaliwa Mama tee wangu. Nakupenda sana na
unalifahamu hilo, natumai umeipenda nyumba yetu hii mpya South Africa.
Nasubiria kwa hamu kusheherekea nawe siku yako hii kubwa kesho (leo) Zanzibar,” Diamond aliandika instagram.
Muimbaji huo
amevunja zile tetesi za kwamba huwenda hayupo sawa na mama Tiffah baada ya
mrembo huyo siku chache zilizopita kudai amekuta hereni za mwanamke mwingine
chumbani kwake.
No comments:
Post a Comment