Jeshi hilo limewataka pia raia
kujiepusha kuwa katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi.
Limesema njia za kutoka katika
maeneo yanayoshikiliwa na waasi zimewekwa wazi kuruhusu watu kutoka.
Tangazo hilo limekuja siku chache
baada ya kushambuliwa kwa eneo hilo linalodhibitiwa na waasi, mashariki mwa
Allepo.
Katika hatua nyingine Marekani na
Urusi zimeshindwa kukubaliana jinsi ya kuufufua upya mkataba wa kusitisha
mapigano, nchini Syria.
Akizungumza baada ya mkutano wao
mjini New York, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry amesema
Urusi inatakiwa kuonesha umakini wake katika kumaliza ghasia nchini Syria.
''.. Iwapo Urusi itatujia na
mapendekezo yenye kujenga tutawasikiliza. Watu wanahitaji kuamini kwa vyovyote
vile inastahili kubadilisha mbinu za upigaji mabomu uliopo sasa ambazo zinaleta
maafa na zenye kutatiza, kwa kubadili mbinu hizo tunaweza kupata ufumbuzi...''
Amesisitiza kuwa njia pekee ya
kuonesha uaminifu ni kuacha mashambulizi ya nga, vinginevyo amesema mazungumzo
mengine yatakuwa hayana msingi.
No comments:
Post a Comment