Wamarekani wamekuwa wakiamini kuwa
Urusi ndio iliyoshambulia msafara huo, huku Warusi wakilipinga hilo.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa
Urusi John Kerry, alitoka nje ya lugha ya kidiplomasia kwa kutumia dhihaka
zaidi. Huku mwenzake wa Urusi Sergey Lavrov akipinga hisia hizo kali kwa
kuorodhesha mifano kadhaa kutetea nchi yake. Aidha ametaka pia kufanyika
Licha ya majibizano makali, Urusi
na Marekani zilikubaliana kwa pamoja kuongoza mkutano wa mataifa 23,
yanayoiunga mkono Syria ambao utafanyika mjini New York, baadaye leo.
Katika hatua nyingine Umoja wa
Mataifa umesema unajiandaa kuanza tena kutoa misaada ya kibinadamu katika
maeneo yaliyozingirwa nchini Syria, baada ya kusitishwa kwa usambazaji wa
misaada kufuatia shambulio hilo.
Mjumbe wa Umoja wa Mnataifa nchini
Syria, Staffan de Mistura ameiambia BBC kwamba misafara hiyo ya misaada itaanza
katika baadhi ya maeneo lakini kwa uangalifu na tahadhari kubwa. Misaada hiyo
amesema haitasambazwa katika eneo linaloshikiliwa na waasi la Aleppo, ambalo
limeshambuliwa vibaya.
No comments:
Post a Comment