
Wakala ya Mkemia Mkuu wa Serikali
imekusudia kuendesha kampeni maalum ya kupima matumizi ya vilevi kwa madereva
wanaosafirisha abiria na mizigo ikiwa ni hatua ya kukabiliana na tatizo la
ajali za barabarani nchini.
Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es
Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele alipokuwa
akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wadau wa kemikali juu ya matumizi salama ya
kemikali nchini.
Profesa Manyele alisema utaratibu
wa kuwapima madereva hao utaanza hivi karibuni na utawezesha kupunguza tatizo
la ajali barabarani na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama kutoa ushirikiano
katika zoezi hilo.
“Madereva wote wanaosafirisha
mizigo na abiria watatakiwa kupita kwenye kipimo ambacho kitaonyesha kama
madereva hao wanatumia vilevi, hali hiyo itasaidia kutatua tatizo la ajali za
barabarani nchini”,alisema Manyele.
Profesa Manyele alisema kuwa
lengo la mafunzo hayo ni kutoa uwezo na uelewa kwa wahusika hasa
wasimamizi wa shughuli za kemikali na matumizi salama juu ya kukabiliana na
matukio au ajali za kemikali pale yanapotokea.
No comments:
Post a Comment